Maisha Na Cancer

Jifunze yote kuhusu saratani ya shingo ya uzazi na HPV Hapa

UFafanuzi

Je, Saratani ya shingo ya uzazi ni nini?

Saratani (Cancer) ni ugonjwa unaosababishwa na mgawanyiko usiodhibitiwa wa seli za mwili na kusababisha uvimbe.

Saratani ya shingo ya kizazi ni: 

  • Saratani inayopatikana popote kwenye shingo ya kizazi, ambayo ni mwanya kati ya uke na tumbo la uzazi.
  • Saratani ya 4 kwa wingi duniani
  • Saratani ya 2 kwa wingi nchini Kenya
  • Saratani ya 2 ya mara kwa mara kati ya wanawake kati ya miaka 15 na 44.
  • Katika kila dakika 2, mwanamke hufa kutokana na saratani ya shingo ya kizazi
  • Kwa kila kesi 1000 za saratani ya shingo ya kizazi, 997 husababishwa na maambukizi ya HPV

SHingo ya njia ya kizazi

MAMBO ya hatari / RISK FACTORS

Je, ni mambo gani yanayoweza kumfanya mtu apatikane na saratani ya shingo ya njia ya uzazi?

  1. Kuwa na maambukizi (infection) ya HPV kwa muda mrefu.
  2. Historia yako ya ngono inaweza changia pakubwa. 
  3. Mifumo ya chini ya kinga kama vile kutoka kwa HIV. 
  4. Lishe ya chini ya matunda na mboga.
  5. Hali ya chini ya kiuchumi ya kijamii.
  6. Umri wa kukua.
  7. Uzito wa ziada wa mwili.

HISTORIA YA NGONO

Je, historia ya ngono inachangia vipi kwa uwezekano wa kupata saratani ya shingo ya njia ya uzazi?

  1. Kuanza ngono mapema / umri mdogo
  2. Kufanya ngono bila kinga
  3. Kufanya ngono na wapenzi wengi
  4. Kufanya ngono na mtu aliye na wapenzi wengi wa ngono

ISHARA NA DALILI / SIGNS AND SYMPTOMS

Je, dalili za saratni ya shingo ya uzazi ni zipi?

  • Kuvuja damu ya uke isiyo ya kawaida 
    • Baada ya ngono
    • Baada ya mazoezi
    • Kati ya hedhi
    • Baada ya kukoma hedhi
  • Muda mrefu wa hedhi nzito
  • Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
    • Majimaji
    • Rangi ya kahawia nyekundu
  • Harufu isiyo ya kawaida
  • Kuongezeka kwa kutokwa
  • Kuvimba, uchungu, muwasho na usumbufu kwa sehemu nyeti
  • Uchungu/taabu wakati wa kukojoa

KUZUIA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI

Jinsi ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi

  • Wanawake wanapaswa kuchunguzwa saratani ya shingo ya kizazi kila miaka 5-10 kuanzia umri wa miaka 30.
  • Wanawake wanaoishi na HIV/VVU wanapaswa kuchunguzwa kila miaka 3 kuanzia umri wa 25.
  • Mkakati wa kimataifa unahimiza angalau uchunguzi utendaji wa juu wa HPV mara mbili maishani kwa kila mwanamke wa umri wa miaka 35 na tena kwa miaka 45. 
  • Precancers mara chache husababisha dalili, ndiyo sababu
  • Uchunguzi wa mara kwa mara wa saratani ya shingo ya kizazi ni muhimu, hata ikiwa umechanjwa dhidi ya HPV.

MATIBABU

  • Upasuaji: Hii inahusisha kuondoa tishu za saratani au kizazi kizima na uterasi. 
  • Tiba ya mionzi: Hii hutumia miale yenye nguvu nyingi kuua seli za saratani au kuzizuia kukua.
  • Chemotherapy: Inalenga kuua seli za saratani au kuzizuia kugawanyika.
  • Tiba inayolengwa: Hii hutumia dawa zinazolenga vipengele maalum vya seli za saratani, kama vile
    protini au jeni. 
  • Immunotherapy: Hii hutumia dawa zinazochochea kinga ya mwili kupambana na saratani seli. 
  • Majaribio ya kimatibabu: Tafiti zinazojaribu matibabu mapya au mbinu za kuzuia au utambuzi. 
  • Utunzaji wa ufuatiliaji: Uchunguzi wa mara kwa mara na vipimo vya kufuatilia majibu matibabu na kugundua dalili zozote za kujirudia au athari.

UFAFANUZI WA HPV

  • Kikundi ya virusi 150 na zaidi. 
  • Inasababisha maambukizi kwa sehemu mbali mbali za mwili.
  • Hatari ndogo(low risk) – yanasababisha maambukizi ndogo. 
  • Hatari kubwa (high risk) – yanasababisha maambukizi kama cancer.
  • Virusi ni viumbe vidogo vinavyoweza kuambukiza viumbe hai, hutegemea kiumbe hicho kwa ajili ya kuishi.

MAMBO YA HATARI

  • Ngozi iliyoharibiwa.
  • Upungufu wa kinga mwilini.
  • Ngono isiyo salama uingiliaji wa ngono wa umri mdogo. 
  • Wanaume wasiotahiriwa. Wapenzi wengi wa ngono

UAMBUKIZAJI WA HPV

  • Kupitia mgusano wa kikaribu (mguso wa ngozi hadi ngozi)- warts kwenye ngozi.
  • Zinaa hasa vijana

CHANJO YA HPV

  1. Virusi kama chembe ambayo hushawishi mwili kutoa mwitikio wa kinga.
  2. Haiwezi kusababisha maambukizi au saratani.
  3. Hutoa mwitikio bora wa kinga kuliko maambukizi.
  4. Inalinda dhidi ya saratani tofauti na warts
  • Cervarix – hulinda dhidi ya saratani.
  • Gardasil 4 – hulinda dhidi ya saratani na warts.
  • Gardasil 9 – hulinda dhidi ya saratani na warts

MIONGOZO YA CHANJO YA HPV

  1. Wasichana kati ya miaka 9 na 14. 
  2. Kinga kamili kabla ya kuanza ngono.
  3. Ikiwa kipimo cha kwanza
    1. kabla ya miaka 15- dozi 2, miezi 6 tofauti.
    2. Ikiwa kipimo cha kwanza kabla ya miaka 15-dozi 2, miezi 6 tofauti. 
    3. Kwa watu wanaoishi na HIV – dozi 3. 
  4. Watu wazima pia wanaweza kupokea chanjo, hadi miaka 26. 
  5. Wavulana pia wanaweza kupokea chanjo, ingawa haiko katika ratiba ya KEPI 
  6. Umri bora wa Chanjo ni kati ya miaka 9 na 12

MALENGO YETU

Utumiaji wa chanjo ya HPV bado iko chini nchini Kenya.

  • 2022 – Asilimia 58% ya wasichana wenye umri wa miaka 10 walichanjwa dhidi ya HPV. 
  • Lengo la 2024 ni asilimia sabini (70%).
  • Lengo la 2026 ni asilimia themanini (80%).

Mkakati wa Kimataifa wa kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi:

  • Asilimia tisini (90%) ya wasichana kuchanjwa kabla ya miaka 15.
  • Asilimia sabini (70%) ya wanawake kuchunguzwa kwa mtihani wa utendaji wa juu kwa miaka 35 na tena katika miaka 45.
  • Asilimia tisini (90%) ya wanawake walio na ugonjwa wa kizazi kutibiwa

MWITO WA KUCHUKUA HATUA

  • Pata taarifa kuhusu saratani ya shingo ya uzazi. 
  • Pata taarifa kuhusu virusi vya hpv na chanjo ya HPV.
  • Nenda kwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.
  • Zuia saratani ya shingo ya kizazi kwa kupata chanjo.